Kundi la wananchi wenye hasira wamevamia kituo cha Polisi Kibiti
Wilayani Rufiji na kuleta vurugu kubwa kutokana na raia mmoja kufa kwa
kile kilichodaiwa kuwa kipigo cha Polisi. Aliyefariki ni Hamis Mpondi
ambaye mauti yamemfika wakati akipatiwa matibabu Muhimbili.
Habari za sasa ni kwamba wananchi hao wanateketeza nyumba za Askari
Polisi zilizopo jirani na kituo hicho licha ya juhudi za Polisi
kuwatawanya kwa mabomu, pia wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu
ya Kilwa iendayo Mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe magogo na
kuchoma matairi ikiwa ni umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha
Polisi Kibiti, hali inaelezwa kuwa inazidi kuwa tete huku Polisi wa
Kibiti wakiendelea na jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua
mabomu hewani kujaribu kutawanya watu.