BREAKING NEWS: WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA ST. JOHN WAANDAMANA KUELEKEA KWA MKUU WA MKOA WA DODOMA


 Maaskari wakiongoza msafara wa wanachuo ambao walikuwa wanaelekea kwa mkuu wa mkoa
 
 Maaskari wakiwa kwenye ulinzi wakati wa maanadamano ya wanachuo waliokuwa wanaelekekea kwa mkuu wa mkoa Dodoma
 Wanachuo wakiwa wameshika mabango ya kushinikiza ulinzi katika chuo cha St. John
 Wanachuo wa chuo kikuu wakiwa kwenye maandamano
 Maaskari wakiwa nyuma ya maanadamano ya wanachuo wa chuo kikuu cha St. John
Wanachuo wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwa mkuu wa mkoa hii ni kushinikiza ulinzi kwa sababu ya matukio ambayo yanaendelea kutokea maana juzi alifariki mwanachuo na usiku wa kuamkia leo wanachuo walivamiwa kwenye chumbani baada ya kukata nindo ya dirisha na kuiba Laptop tatu na simu tano na baada ya kuchukua vitu hivyo waliacha wamewafanyia vitendo vibaya na pia waliachwa wamefungwa ili wasipige kelele.
Kwa hali hii  imesababisha maandamano ili kushinikiza ulinzi katika chuo cha St. John kilichopo Dodoma mjini.
 
Wanafunzi hao ambao waliandamana umbali wa kilomita tatu leo kutoka chuo kilipo na kuishia viwanja vya Mwalimu Nyerere walidai wanalenga kufikisha ujumbe kwa jamii kutambua vitendo vya kikatili vinavyofanyika chuoni hapo.
Maandamano hayo ambayo yalikuwa yakisindikizwa na
Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia, yalipita katika mitaa mbalimbali ya Manispaa ya Dodoma.

Waandamanaji hao ambao mbali na kuimba nyimbo za kulilaumu Jeshi la Polisi kwa kushindwa kuthibiti vitendo hivyo, pia mabango waliyokuwa wamebeba yalikuwa yakililaumu jeshi hilo.
 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo