KATIBU WA CCM MUFINDI AFIKISHWA MAHAKAMANI AKITUHUMIWA KUTISHIA KUUA



 .

Na Francis Godwin


KATIBU  wa chama  cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jackob Nkomola leo amefiishwa mahakamani akituhumiwa  kuua kwa maneno .

Akisoma shtaka hilo  linalomkabili katibu  huyo  mahakamani hapo hakimu  wa mahakama ya mwanzo Mafinga wilayani Mufindi Zakaria Mushi alisema  mtuhumiwa Jackob Nkomola anashtakiwa kwa kosa la kumtishia kumuua  kwa maneno, Alexandel Tweve  kinyume na  sheria kifungu namba 89 kifungu kidogo “A”.

Aidha hakimu huyo alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo, Octoba 3 mwaka 2012 katika eneo la Mkombwe, ambapo alimtishia mkazi huyo wa mji
  wa Mafinga  wilaya ya Mufindi..

Mtuhumiwa alikana shtaka hilo na hakimu kutoa masharti ya dhamana ya ahadi
  ambayo inathamani ya shilingi  200,000 na adhaminiwe na mtu mmoja atakayetambulishwa kwa barua kutoka katika ofisi ya serikali ya kijiji au Kata masharti ambayo yalitimizwa na mshitakiwa na kesi hiyo itafikishwa  tena mahakamani hapo Januari 30 mwaka huu.

Hakimu alimtaka mlalamikaji   wa kesi hiyo kufika na mashahidi wake

aliowaorodhesha.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo