HAWAJAWAHI KUTEMBELEWA NA RAIS WALA WAZIRI TOKA NCHI IPATE UHURU 1961

                                       Rais Jakaya  Kikwete
  NA FRANCIS GODWIN
WANANCHI  wa kata  ya Ludende jimbo la  Ludewa  mkoani Njombe wadai  toka nchi ipate  uhuru mwaka  1961 katika kata   hiyo hawajapata  kutembelewa na Rais wala  waziri japo wamekuwa  wakibahatika  kuona  picha za Rais na  mawaziri  kwenye magazeti pekee.

Wakizungumza  katika  mkutano  wa hadhara  wa mbunge wa  jimbo  hilo la  Ludewa Deo Filikunjombe juzi  wananchi hao   walimwomba  mbunge huyo  kufikisha ombi lao la  kutembelewa na viongozi hao  wa  juu kwa Rais Jakaya  Kikwete  ili ikiwezekana kabla ya  kumaliza  muda  wake  kuwatembelea  wananchi hao.

Fidelis Haule  alisema  kuwa yawezekana  kata  hiyo  imeendelea  kua  nyuma  katika  maendeleo kutokana na viongozi  wa  ngazi ya  juu  serikali  kuitenga  kata  hiyo .

Alisema  kuwa kwenye kata  hiyo ambayo  wananchi  wake  wamekuwa  wakilazimika  kutumia maji ya mto na madimbwi ya mvua   kutokana na  kutokuwa na  huduma ya maji   safi na salama  pia  inakabiliwa na matatizo mbali mbali  likiwemo tatizo la daraja  linalounganisha kijiji  hicho na  vijiji vya jirani .

Haule  alisema  kuwa  viongozi wa  Halmashauri ya  wilaya  hiyo ya  Ludewa  wameendelea  kuwa  kikwazo   kikubwa  katika maendeleo ya kata  hiyo na wameendelea  kukwama katika  uzalishaji  kutokana na utendaji mbovu  wa  viongozi wao.

Kwani  alisema  pamoja na maeneo mengi ya wilaya  hiyo  wakulima  wameanza  kupalilia mahindi  yao  ila katika  kata  hiyo baadhi ya  wananchi bado hawajapanda mazao yao  walikuwa  wakisubiri mvolea  hiyo ya  ruzuku.

Kwa  upande  wake katibu wa itikadi na uenezi    wa chama  cha mapinduzi (CCM) mkoa  wa Njombe Honoratus Mgaya  alisema  kuwa  wananchi hao  wanahoja ya  msingi kuhusu viongozi  wao  ila aliwataka  kuondoa  hofu na kuwa Rais anawakilishwa na mkuu  wa  wilaya  kwa  upande wa  serikali na upande wa chama  mbunge  ni mwakilishi  wa Rais pia kwa maana ya mafiga matatu ya CCM kwa maana ya  diwani, mbunge na Rais.

Hata  hivyo  alisema  kuwa iwapo  wilaya  hiyo ya  Ludewa  pekee  inazaidi ya  vijiji 77 na kata  zaidi ya 25 kwa  upande wa Tanzania  nzima  kuna zaidi ya  vijiji vingi  zaidi na hivyo  wasilalamike kwa Rais  kutofika  kata   hiyo na kuwa  ip  siku atafika ama waziri .

Mbunge   wa    jimbo  hilo la Ludewa Filikunjombe  alisema kuwa kwa upande  wake  kama mbunge anaendelea  kupambana na utatuzi  wa  kero  mbali mbali  zinazowakumba  wananchi hao


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo