Waumini wa Jimbo la Arusha Magharibi ndani la
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini kati
wametishia kujitenga iwapo masharti yao hayatatekelezwa.
Masharti hayo ni pamoja na kuwataka viongozi waandamizi wa Dayosisi hiyo, akiwamo Askofu Thomas Laizer na Katibu Mkuu wa Dayosisi, Israel Karyongi kujiuzulu kutokana na tuhuma za ufisadi wanazozielekeza kwao.
Sambamba na viongozi hao kuachia nyadhifa zao, waumini hao pia wanataka Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Ngateu katika jimbo hilo, Philemon Mollel, arejeshewe uchungaji wake mara moja bila masharti yoyote.
Mchungaji Mollel ambaye amekuwa mstari wa mbele kutetea na kupigania mali za Dayosisi hiyo, amefukuzwa kazi na kuvuliwa uchungaji ndani ya kanisa hilo.
Hatua ya kuwataka viongozi hao waandamizi wa Dayosisi kujiuzulu na kurejeshewa uchungaji wake Mchungaji Mollel ilifikiwa juzi katika kikao cha viongozi wa sharika mbalimbali za Jimbo la Arusha Magharibi pamoja na wazee waliokutana jijini hapa kujadili mustakabali wa Dayosisi hiyo.
Mmoja wa viongozi wa jimbo hilo ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini, alithibitisha kuwapo kwa tamko hilo akisema kuwa wachungaji waliohudhuria kikao hicho wapo tayari kujitenga na Dayosisi ya Kaskazini Kati endapo

uamuzi wao hautafanyiwa kazi.
‘’Hali ni tete wala tusijidanganye, waumini hawaelewi kinachoendelea na kinachofuata ni sisi kujitenga na Dayosisi kwa kuwa ufisadi, udikteta na ufujaji ovyo wa mali za Dayosisi unazidi kuongezeka kila kukicha,’’ alisema na kuongeza:
“Watu wanapigania wahusika katika kufuja mali za kanisa wawajibishwe lakini wengine wachache wanawaunga mkono kwa maslahi yao huku wengine wakitolewa kafara... Kamwe hatutakubali haya yafanyike kanisani.”
Juhudi za kumpata Askofu Laizer na Katibu Mkuu wa Dayosisi, Karyongi hazikuzaa matunda, kwani simu zao ziliita bila kupokewa na hata walipotumiwa ujumbe wa simu uliotaka ufafanuzi juu ya hatua hiyo ya waumini, hakukuwa na majibu.
Hata hivyo, Mkuu wa Jimbo la Arusha Magharibi, Mchungaji Godwin Lekashu, alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa hatua hiyo alisema: “Mimi kama Kiongozi wa Jimbo sina taarifa rasmi ya kikao hicho, na kama kingekuwa rasmi ningekuwa na taarifa na hata maamuzi yake ningeyafahamu.” “Kwa ufafanuzi zaidi ningekushauri uwasiliane na msaidizi wa Askofu ambaye ndiye msemaji wa Dayosisi ya Kaskazini Kati,” alisisitiza Mchungaji Lekashu ambaye inaelezwa kwamba ni mfuasi mkubwa wa Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo.
Jana, vurugu, mabishano na ubabe vilitawala katika Usharika wa Ngateu, baada ya Askofu Msaidizi wa Dayosisi hiyo, Solomon Massangwa na ujumbe wake, kuwasili kujaribu kueleza hali halisi ya mgogoro unaofukuta ndani ya Kanisa hilo.
Lakini tofauti na matarajio yao, walikumbana na upinzani mkali kutoka kwa waumini waliopinga kikao cha siri baina ya msaidizi wa Askofu na ujumbe wake, uliolenga kukutana na wazee wa Usharika huo.
Akifuatana na Mchungaji mstaafu Gabriel Kimerei na Katibu wa Jimbo la Arusha Magharibi la Dayosisi hiyo, Daniel Medani, Askofu huyo Msaidizi alikutana na umati wa waumini waliokuwa katika makundi kwenye viwanja vya Kanisa hilo, ndipo akaomba kuonana na wazee wa Kanisa. Hata hivyo, wakati akiomba kukutana na wazee, waumini walicharuka na kutaka kusiwe na kikao cha siri.
Masangya aliwaambia waumini hao ya kuwa amefika kanisani hapo kusikiliza kero yao na kuwataka watulize jazba, kitendo ambacho kilipingwa vikali.
Hatahivyo, mara baada ya mvua kunyesha kwa wingi aliwashauri waumini hao waingia ndani ya kanisa lao ili waweze kufanya kikao hicho kwa utulivu kitendo kilichopokelewa na kisha waumini hao kuingia ndani ya kanisa hilo.
Akiwa ndani ya kanisa hilo msaidizi huyo aliibua gumzo mara baada ya kuwaambia ya kwamba anaomba akutane na baraza la wazee wa usharika huo na kisha baadaye atawapa taarifa ya kile kilichojadiliwa.
“Jamani ndugu waumini nawaomba mtoke nje ili nikutane na baraza la wazee wa usharika wenu halafu tukimaliza kuongea nao tutawapa taarifa kamili,” Masangya alisikika akiwaambia waumini
Hatahivyo, waumini hao walipinga wazo hilo kwa madai kwamba hakuna usiri wowote katika jambo hilo na kitendo cha kutaka kukutana na baraza hilo ni kutaka kuficha baadhi ya mambo ambayo wamekuwa na wasiwasi nayo, ‘’Hakuna kuzungumza na wazee wakati kila kitu kiko wazi, semeni mbele yetu na mtueleze Mchungaji Mollel (Philemon) anarudi lini kazini na waliosababisha mambo kuharibika wanawajibika vipi?’’ alisema Zephania Kwayu, mmoja wa waumini hao na kiongozi wa Kwaya ya Usharika huo.
Kauli ya Kwayu iliwapandisha mori waumini wengine ambao nao walipiga kelele kwa sauti za juu kwamba hawataki kusikia chochote zaidi ya Mchungaji Mollel kurudishwa kazini mara moja na bila masharti.
Wakionekana wazi kukasirika, waumini hao jana walikaribia kuchukua sheria mkononi kwa kutaka kumshambulia Askofu Massangwa ambaye alilazimika kujificha katika ofisi za Usharika huo kupitia mlango wa nyuma wa Kanisa hilo.
Mara baada ya vuta ni kuvute hiyo ndipo katika hali isiyo ya kawaida Askofu mstaafu, Kimerei aliamua kuamka na kutangaza ya kwamba kikao hicho kimehairishwa, jambo ambalo lilichafua hali ya hewa kanisani hapo.
Baadhi ya waumini waliokuwepo ndani ya kanisa hilo walianza kuwazomea viongozi hao wa kiroho na wengine wakionekana wakifunga milango ya kanisa hilo ili wasitoke nje hali iliyopelekea viongozi hao kukimbizwa katika moja ya ofisi zilizopo ndani ya kanisa hilo kwa muda.
Huku waumini wengine wakifunga milango ya Kanisa ili Askofu huyo na ujumbe wake wasitoke, mvua kubwa ilinyesha hali iliyosaidia kuwaokoa na kipigo cha washarika wao, “Fungeni milango yote asitoke huyo, wamezoea kulinda mafisadi na tunataka Mchungaji wetu arudishwe haraka, la sivyo tuwafundishe adabu hapa hapa kanisani,’’ washarika hao walisikika wakifoka kwa sauti za hasira huku wakiwa tayari kwa lolote.
Jitihada za baadhi ya wazee wa Usharika huo kuwatuliza waumini wao hazikuzaa matunda, huku ujumbe huo ukitoroshwa ili kuokoa maisha yao licha ya mvua kubwa kuwanyeshea.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya waumini wa kanisa hilo walisema ya kwamba endapo mchungaji wao asiporudishwa kuongoza kanisa hilo patachimbika.
Waumini hao walidai kwamba wako tayari kujitenga na kuanzisha dhehebu lao huku wakitangaza msimamo wa kutopeleka sadaka zao mbele ya dayosisi hiyo kwa madai kwamba kuna wamenusa harufu ya ufisadi.
“Kuanzia leo hatupeleki sadaka yoyote dayosisi na tunataka mchungaji wetu atuongoze kwenye sadaka ya mwaka mpya hatumtaki mchungaji yoyote wakitulazimisha patachiumbika hapa ni bora tujitenge,” walisema kwa nyakati tofauti.
Baada ya Askofu Msaidizi kufanikiwa kutoroka na ujumbe wake, Kwayu aliwaambia waumini kwamba wametoa hoja kumi za kutekelezwa na viongozi wa Dayosisi ili kurudisha mshikamano kanisani humo.
Moja ya hoja hizo ni pamoja na kurudishwa kazini Mchungaji Mollel, kufukuzwa kazi mara moja kwa Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Israel ole Karyongi na kujiuzulu kwa Askofu wa Dayosisi hiyo, Thomas Laizer.
Mgogoro ndani ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati uliibuka baada ya waumini kupewa waraka wa kutakiwa kila mmoja kuchangia Sh 20,000 ili kunusuru mali za Kanisa zilizo hatarini kufilisiwa baada ya hoteli ya Corridor Springs kudaiwa Sh bilioni 11 na benki moja nchini.
Hatua hiyo inapingwa na waumini hao na baadhi ya wachungaji akiwamo Mollel anayetaka wahusika wa kadhia hiyo wachukuliwe hatua; lakini ‘aligeuziwa kibao’ na kufukuzwa na kuvuliwa madaraka ya kutoa huduma za kichungaji katika Kanisa hilo nchini.
Vyanzo vyetu vya habari ndani ya Kanisa hilo vilieleza kuwa hatua hiyo ilitokana na Mchungaji Mollel kushindwa kutekeleza mambo matatu aliyotakiwa na Tume maalumu ya watu watatu walioteuliwa na Menejimenti ya Dayosisi hiyo na alipewa siku tatu kuomba radhi, lakini hakufanya hivyo.
Habari zilieleza kuwa walioteuliwa Desemba 14 na kwenda kumwona Mchungaji Mollel kutekeleza hayo ni pamoja na Massangwa, Katibu Mkuu wa Jimbo la Arusha Magharibi, Mchungaji Godwin Lekashu na Karyongi.
Taarifa za ndani zilisema Mchungaji Mollel aliandikiwa barua Desemba 17 na kutakiwa kufanya mambo hayo matatu kabla ya Desemba 23.
Mosi, alitakiwa kumwandikia barua Askofu Laizer kumwomba radhi na kueleza ni kwa nini alimkashifu na kumdharau. Pili, atoe tamko katika Mtaa wa Azimio ibadani Desemba 23, akiomba radhi kwa aliyotamka; Tatu ifikapo Desemba 23, awe amemwarifu Katibu Mkuu kwa barua kuhusu utekelezaji wa maagizo hayo na kwamba yote yafanyike kabla ya Desemba 24, 2012.
Vyanzo vya habari vilisema baada ya Mchungaji Mollel kukaidi hayo, kikao cha watu watatu wakiongozwa na Karyongi kiliamua kumfukuza kazi na kumvua uchungaji. Hata hivyo, habari za uhakika zilisema Mchungaji Mollel hakufanya hivyo kwa madai kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu aliyetukuka kufuata maadili na kamwe hawezi kufanya hivyo, kwani hakumkashifu mtu wala kiongozi yeyote, bali alieleza ukweli juu ya nani wa kuwajibika katika deni la Sh bilioni 11.
Wakati huo huo, habari zilizotufikia baadaye jana zilieleza kuwa, Askofu Laizer amelazwa katika hospitali maarufu ya Kanisa hilo ya Selian, mjini Arusha. Chanzo cha habari kilisema alilazwa tangu juzi. Juhudi za kumwona hospitalini hapo hazikuzaa matunda kutokana na kutanda kwa usiri wa kulazwa kwake. Inadaiwa anasumbuliwa na shinikizo la damu.
---
Habari via gazeti la HabariLeo na blogu ya Pamela Mollel (habari iliyoandikwa na Moses Mashallah)