Vijana wa Manispaa ya Iringa wakifukua makaburi ya Igumbilo kupisha mradi wa umeme Iringa- Shinyanga |
Vijana wakitazama mabaki ya mwili wa binadamu baada ya kuchimba moja kati ya kaburi eneo hilo la Igumbilo |
Vijana wengi wamejitokeza kuifanya kazi hi |
Mmiliki wa mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com mzee wa Matukio daima (kulia) akimtazama mmoja kati ya vijana ambao wanafanya kazi ya kufukua makaburi eneo la Igumbilo mjini Iringa ,kaburi moja wanafukua kwa shilingi 70,000 |
BAADHI ya vijana wasio na ajira katika Manispaa ya Iringa mkoani Iringa leo wamejitokeza kwa wigi katika eneo la Igumbilo mjini Iringa kufukua mabaki ya miili ya watu waliozikwa katika makaburi ya Igumbilo ili kupisha mradi mkubwa wa umeme unaotarajiwa kupitia eneo hilo kuelekea mkoa wa Shinyanga .
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia vijana zaidi ya 50 ambao wamekuwa wakishinda vijiweni wakigombea kufukua makaburi ya zamani na kutoa mabaki ya miili hiyo na kwenda kuizika katika eneo jipya ambalo limetengwa na uongozi wa serikali ya kijiji cha Igumbilo ambalo ni eneo la jirani na eneo hilo la awali.
Wakizungumza kwa sharti ya kutotaja majina yao vijana hao ambao baadhi yao ni wanafunzi wa vyuo vya ufundi na shule za sekondari mjini Iringa wamedai kuwa kati ya shughuli ambazo zimeweza kuwapatia fedha za haraka zaidi ni pamoja na mradi huo wa umeme ambao umetoa ajira kwa vijana wengi zaidi.
Vijana hao walisema kuwa wamekuwa wakilipwa kati ya shilingi 40,000 na shilingi 70,000 kwa siku kwa kuchimba na kufukua kaburi moja hivyo kutokana na mradi huo wa umeme wameweza kunufaika zaidi.
"Kweli huu mradi umetusaidia sana vijana tusio na kazi ya kufanya kwani hapa leo ukichimba kaburi moja unalipwa shilingi 40,000 wakati mfukuaji wa kaburi na kuzika ni shilingi 70,000 kwa siku....hadi sasa vijana tunagombea kuchimba na kufukua makaburi haya "
Hata hivyo vijana hao walisema kuwa wamekuwa wakiifanya kazi hiyo kwa hofu kubwa kutokana na kuwepo kwa taarifa za imani za kishirikina kuwa badhi ya maeneo kama hayo ya makaburi huwa kunatokea mauza uza wakati wa kuhamisha makaburi japo katika eneo hilo hadi sasa hawajakutana na mauza uza yoyote.
Afisa afya wa Manispaa ya Iringa Sevelin Tarimo ambae amekuwa akisimamia shughuli hizo za ufukuaji na uzikaji wa mabaki ya miili hiyo alisema kuwa taratibu zote za mazishi pamoja na zile za haki ya binadamu katika kuhifadhiwa zimekuwa zikifuatwa katika zoezi hilo.
Tarimo alisema kuwa ndugu wa marehemu waliozikwa katika maeneo hayo wote wamelipwa fidia na kuruhusu makaburi hayo kuhamishwa na kuwa hadi sasa zoezi kama hilo limefanyika eneo la Nduli ,Kigonzile na eneo hilo la Igumbilo.