
Afisa
habari wa mkoa wa Dar es salaam Bi. Adrofina Ndyeikiza akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kwa niaba ya mkuu wa mkoa
huo kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambayo kimkoa
yatafanyika katika uwanja wa Biafra, Manispaa ya Kinondoni. Kulia ni
Mratibu wa Ukimwi wa Mkoa wa Dar es salaa kutoka TACAIDS Bw. Omary
Chambo.

Mratibu
wa Ukimwi wa Mkoa wa Dar es salaa kutoka TACAIDS Bw. Omary Chambo
akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu hali ya maabukizi ya
ugonjwa huo katika jiji la Dar es salaam na kutoa wito kwa wakazi wa
jiji hilo kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali katika kupambana
na Ugonjwa huo.