Hivi ndivyo basi La Abood lilivyo pata ajali baada ya kugongana na Kenta
Basi la Abood
Hivi ndivyo Basi Lilivyo Haribika
Haya ni mambaki ya Vioo vilivyo vunjika
Baadhi ya vitu vikiwa vimemwagika chini
Hili ni Scania ambalo lilikuwa likitokea Zambia
Dirisha likiwa limevunjika
Baadhi ya Abiria wakiwa wanapata maelekezo kutoka kwa polisi
Hapa ndipo basi la Abbod lilipo gonga
*********************
BASI LA ABOOD LENYE USAJILI WA NAMBA T 545 AZE LIMEPATA AJALI MAENEO YA SAE SEHEMU MAARUFU KWA JINA LA KWA MBILINYI LIKITOKEA DAR ES SALAAM KUELEKEA TUNDUMA.
AJALI HIYO IMETOKEA BAADA YA LORI LA MIZIGO AINA YA SCANIA LIKIWA LIMETOKEA ZAMBIA KUELEKEA DAR WAKATI WA KUTAKA KUPISHANA NA BASI HILO, NA NDIPO GARI AINA YA KENTA IKAJITOKEZA NA KUJICHOMEKA BARABARANI NA KUSABABISHA AJALI HIYO.
KATIKA AJALI HIYO MTU MMOJA AMBAYE ANAITWA CHALE KITELEKE AMBAYE PIA ALIKUWA NDIYE KONDA WA BASI HILO AMEFARIKI PAPO HAPO, PAMOJA NA MAJERUHI NANE AMBAO WAMEKIMBIZWA HOSPITALINI .
HABARI KAMILI ITAWAJIA BAADA YA KUPATA TAARIFA KUTOKA POLISI.
PICHA ZOTE NA: MBEYA YETU BLOG