Na mwandishi wetu Hadija Sanga,MAKETE
Mkuu wa shule ya msingi Ludihani iliyopo kijiji cha Ludihani wilayani Makete amesema kuwa ujenzi wa nyumba ya walimu shuleni hapo bado unaendelea.
Akizungumza na waandishi wa habari hii ofisini kwake Mwalimu mkuu huyo Bw. Leo Mahenge ameeleza kuwa ujenzi huo ulianza mwezi wa Machi 2012 mpaka sasa unaendelea vizuri kutokana na nguvu za wananchi wa kijiji hicho.
Bw. Mahenge ameongeza kuwa mpaka sasa ni nyumba moja tu ambayo tayari imekamilika na anaishi mwalimu mkuu huyo na pia ujenzi wa nyumba hiyo umegharimu milioni tatu na laki sita zilizotolewa na mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi [MMEM].
Hata hivyo Bw. Mahenge amezitaja baadhi ya changamoto anazokabiliana nazo shuleni hapo kuwa ni upungufu wa walimu pamoja na uchache wa nyumba za kuishi walimu hao.
“Kweli pamoja na changamoto kwa kweli ni upungufu wa waalimu natambua kuwa ni tatizo la kitaifa lakini waalimu ni muhimu kwa shule yetu serikali inatakiwa iliangalie hili kwani linakwenda sambamba na nyumba za waalimu” alisema
Bw. Mahenge ametoa wito kuwa anaomba serikali kuongeza idadi ya walimu shuleni hapo kutokanana walimu kushidwa kumudu kufundisha idadi ya wanafunzi wote.