JELA MIAKA 14 KWA KUWAFANYIA VITENDO VIOVU WASICHANA


Osezua Osolase
Mwanaume aliyewafanyia vitendo vya kishirikina au ''Juju'' wasichana ambao alikuwa anawalangua kutoka nchini Nigeria hadi barani Ulaya amehukumiwa jela miaka 20 nchini Uingereza.
 
Osezua Osolase raia wa Nigeria na mwenye umri wa miaka 42,kutoka mtaa wa Gravesend, Kent aliwatumia wasichana maskini kwa kuwahadaa kuwa wangepata maisha mazuri baada ya kufika alikokuwa anawapeleka.
Osolase alipatikana na hatia ya makosa matano ikiwemo ubakaji na kumfanyia dhulma za kingono mtoto mdogo.

Jopo la majaji lilisikia katika kesi hii iliyoisha siku ya Ijumaa kuwa vitendo vya kishirikina pia vilitumiwa kuwatia hofu waathiriwa watatu wa vitendo vya Osolase.

Jaji alisema kuwa Osolase ambaye ni mwathiriwa wa HIV, aliwatia hofu waathiriwa wake ili kuwalazimisha kumtii na kukaa kimya.

"umetenda dhulma na kuwafanyia unyama waathiriwa vitendo vyako'' jaji alimwambia bwana Osolase.

"wewe sio mwaminifu hata kidogo. Una kiburi na ukatili, hauna ubinadamu wala huruma kwa waathiriwa wako.'' aliongeza jaji
Aidha jaji Williams alisema kuwa bwana Osolase aliwaharibu wasichana hao wakati alijua kuwa ana virusi vya HIV na hata kumbaka msichana mmoja wakati akijua alifanya kitendo kibaya sana .

Osolase aliwapeleka wasichana hao kwake nyumbani kabla ya kuwapeleka barani Ulaya kufanya kazi ya ukahaba.

Mahakama ilisema kuwa mwanaume huyo arejeshwa nyumbani Nigeria atakapomaliza kuhudumia kifungo chake.

Mmoja wa wasichana alielezea yaliyomkuba wakati akifanyiwa vitendo vya kishirikina, alisema alitolewa damu mwilini , kisha akakatwa nywele zake za kichwani na sehemu zake za siri.Baada ya hapo alilishwa kiapo kutosema chochote.

Osolase alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Stansted mwezi Aprili alipojaribu kupanda ndege mwaka jana.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo