Mwenyekiti wa BAVICHA taifa John Heche akiongea na wanahabari hii leo
Hapa mmiliki wa mtandao huu eddy mo blaze akimhoji Bw. Heche
Hapa mmiliki wa mtandao huu eddy mo blaze akimhoji Bw. Heche
Siku
moja baada ya Mgombea udiwani kata ya Luwumbu wilayani Makete kwa tiketi ya CCM
kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo, Chama cha demokrasia na maendeleo
CHADEMA kimesema kinatarajia kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo muda wowote
kuanzia sasa
CHADEMA
kimesema uchaguzi huo ulitawaliwa na vitendo vya rushwa kwa kiasi kikubwa pamoja
na sababu nyingine tano ambazo wameona kuwa ndizo watazisimamia mahakamani
kupinga matokeo hayo
Akizungumza
hii leo na mtandao huu wa eddymoblaze.blogspot.com mwenyekiti wa baraza la
vijana wa chadema taifa BAVICHA Bw. John Heche amesema wameamua kwenda
mahakamani kupinga matokeo hayo kutokana na sababu tano walizozigundua ikiwemo
sababu kuu iliyofanywa na naibu waziri wa maji na mbunge wa jimbo la Makete
Dkt. Binilith Mahenge
“Tutakwenda
mahakamani tukiwa na sababu kama tano hivi ya kwanza na iliyotushangaza ni ya
naibu waziri kutumia cheo chake kutoa ahadi ya serikali kwenye mkutano wa CCM wa kufunga kampeni pale Usililo kuwa
wakichagua CCM basi atawaletea maji, huu ni ukiukwaji wa taratibu na
hairuhusiwi, nadhani mlisikia aliyosema waziri wa ujenzi pale Igunga sina haja
ya kurudia” alisema Heche
Pia
kiongozi huyo hakutaka kuzitaja sababu nyingine zinazopelekea wao kwenda
mahakamani, ila alizizungumzia kitendo cha watu wachache kujitokeza kushiriki
uchaguzi huo kuwa kwa kiasi kikubwa limechangiwa na rushwa na vitisho
Amesema
kwenye uchaguzi huo kulitawaliwa na aina mpya ya rushwa yaani rushwa ya pombe,
ambapo watu walinunuliwa pombe ili wakichague chama cha CCM ilihali walitakiwa
watoe sera zao na watu wawachague bila kuwapa chochote
Ameongeza
kuwa mbali na na hilo pia ziligawanywa kofia, na t-sherts kwa wananchi hao,
huku akisema kutokana na chama chake kutotambulika sana katika kata hiyo,
wanakwenda kujipanga na watakuja kukiimarisha zaidi wakati wa kampeni ya M4C
katika mikoa ya Iringa na Njombe na Makete ikiwemo
Kwa
upande wao CCM kupitia kwa Katibu wa wilaya Bw. Miraji Mtaturu amesema
waliutegemea ushindi huo tangu mwanzoni licha ya mgombea wao kupakwa matope na
Chadema kwa kumuita fisadi
Amesema
anawashukuru wanaluwumbu kwa kuwa matokeo ya uchaguzi huo yameonesha kuwa
mgombea wao sio fisadi na ndio maana ameshinda kwa kishindo
Amekiponda
chama cha chadema kusema kuwa kina siasa za uongo kwa kuzusha vitu vya uongo
kwa CCm ikiwemo kumuita mgombea wao ni fisadi
“Unajua
kama huna utafiti huna haki ya kuzungumza mtu unasikia tu kuwa Fulani ni fisadi
na wewe unayachukua na kuyapeleka jukwaani kuwa Fulani ni fisadi, hii
haipendezi, tufanye siasa za kisayansi na ndio maana tumewapiga bao tena
kubwaa” alisema Mtaturu
Pia
ameongeza kuwa kutokana na ilani ya CCM kutekelezwa katika kata hiyo kwa sasa
wataendeleza kutekeleza shughuli walizozifanya tangu awali za kielimu na kiafya
ili kuendeleza waliyowaahidi wananchi
Akitangaza
matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Makete Bw. Cyrus Kapinga amesema
idadi ya wapiga kura walioandikishwa walikuwa ni 1,592 lakini idadi ya
waliopiga kura ni 620, kura zilizoharibika 15
Amesema
Mgombea kupitia Chadema Bw. Raphael Kyando alipata kura 40 huku mgombea wa CCM
Mch. Enock Ngajilo akipata kura 565
Mtandao
huu umeshindwa kupata maoni ya wagombea hao kutokana na mgombea wa CCM
kupata msiba wa mwanaye na mgombea wa
chadema kutopatikana kwa simu yake ya kiganjani