MASHIRIKA yanayojihusisha na utoaji wa elimu na misaada kwa watu wenye maambukizi ya Virusi vya ukimwi wilayani Makete Mkoani Njombe yameshauriwa kupeana taarifa wakati wa kutoa huduma kwa watu wenye maambukizi ili kuepusha kuwepo na takwimu sisizo sahihi za idadi ya watu wanao hudumiwa
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa shirika lisilo kuwa la kiserikali la MASUPHA linalo jishughulisha na masuala ya utoaji wa huduma ya elimu kwa watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi Wilayani hapa Bi,Aida Chengula alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,
Amesema kutokana na kuwepo kwa mashirika mengi wilayani hapa yanayofanya kazi zinazo endana za kuwasaidia watu wenye maambukizi kumekuwepo na mkanganyiko katika kutoa takwimu za idadi sahihi za watu wenye maambukizi kutokana na watu wanaopatiwa huduma na mashrika hayo kuwa ni walewale, huku takwimu ziki onyesha kuwa idadi ya watu wenye maambukizi ni kubwa.
Kwa upande wa shirika lake Bi Aida amesema wamekuwa wakiwahamasisha watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi kujiunga katika vikundi ili waweze kupatiwa huduma stahiki ikiwemo kupatiwa mikopo itakayo wasaidia kuanzisha miradi mbalimbali na pia kwa upande washirika inawasaidia kupata idadi sahihi ya watu wanao hudumiwa.
Pi amewataka watu wenye maambukizi kutoa ushirikiano kwa mashirika kwa kutokujiunga katika kikundi zaidi ya kimoja kwani kwa kufanya hivyo kutiwezesha serikali na wahisani kuweza kujua takwimu sahihii,
Aidha amesema shirika lake limeanza mradi wa kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kuwapa mikopo na elimu juu ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi na kwa wale ambao tayari wanamambukizi kujua namna sahihi ya kujilinda na maambukizi mapya.
Shirika la MASUPHA limekuwa likijihusisha na utoaji wa elimu ya matumizi ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi,upimaji na uuandaji wa lishe kwa watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi wilayani hapa tangu mwaka 2005 na kwa sasa lina hudumia watu wenye maambukizi 1200.
Pia nilitaka kujiridhisha kwa kupata takwimu sahihi za watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi wilayani hapa lakini jitihada za kumpata mratibu wa ukimwi na mganga mkuu wa wilaya ya Makete zimeshindikana kwa kuwa walikuwa katika majukumu mengine na kuahidi kunipa takwimu hizo mara watakapomaliza majukumu hayo.