Mradi wa pamoja tuwalee wilayani Makete
umewajengea uwezo zaidi wawezeshaji kutoka katika kata nane za wilaya hiyo juu ya ukatili na unyanyasaji
wa kijinsia unaojitokeza katika kata zao
Akitoa mafunzo hayo mwezeshaji wa haki za
mtoto na kinamama Bi Stela Mdawa amesema lengo la mafunzo hayo ni
kuwajengea uwezo wawezeshaji hao kutoka katika kata nane za Makete ambazo
ni Bulongwa,
Ipepo, Ipelele, Luwumbu, Iwawa, Isapulano na Iniho, na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo wataisaidia jamii
kujikwamua na unyanyasaji wa kijinsia
Amesema unyanyasaji ama ukatili wowote ule
ukiwemo wa kijinsia hupelekea madhara makubwa kwa jamii ikiwemo vifo ama
maamukizi ya virusi vya Ukimwi hasa kwa wanawake ambao ndio waathirika zaidi wa
vitendo hivyo, huku akiwataka washiriki kupeleka elimu waliyofundishwa katika
kata zao
Kwa upande wao washiriki wa warsha hiyo wameonyesha
kufurahishwa na mafunzo hayo na kuahidi kufikisha elimu hiyo kwa wanajamii pamoja na kuunda klabu za watoto ili kusaidia kukomesha
vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya wanajamii hasa kwa kina mama
na watoto
Naye mratibu wa program ya Pamoja Tuwalee
Mchungaji Ezekiel Sanga amesema mradi huo unafadhiliwa na watu wa Marekani kupitia shirika la Africare kwa kushikiana na
asasi ya ELCT Makete unatekelezwa kwa muda wa miaka mitano ijayo katika kata
kumi za wilaya Makete kwa kushirikiana na dawati la unyanyasaji kutoka idara ya
polisi kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kuachana na vitendo vya unyanyasaji na
ukatili
Na RIZIKI MANFRED