Na
Christina Mwagala.
SERIKALI
imekusudia
kuwalipa waathirika 1788 wa mabomu ya mbagala wilayani Temeke jijini
Dar es Salaam shilingi bilioni 2.2 kama fidia.
Hatua
ya kulipwa waathirika hapo imekuja hivi karibuni kutokana
na malalamiko yao kuwasilishwa kwa Serikali
baada ya kuona kuwa walikuwa wamesahaulika.
Akizungumza
jijini
Dar es Salaam jana Mkuu wa Mkoa Said Meck Sadiki alisema waathirika hao
watalipwa Jumatatu.
Aidha
Sadiki alisema kuwa wathirika
2132 ndio walikuwa wakidai
fidia lakini kutokana na tathimini
iliyofanywa imeonekana kuwa wathirika 1788 ndio wanao stahili kulipwa
huku
wengine 344 ha watalipwa kwakile
kilichodaiwa kuwa walishalipwa tangu hapo awali.
Sadiki
alieleza kuwa majina ya watako lipwa fidia
ya tabandikwa kwenye mabango ya serikli za kata huku akiwataka
wahusika watakaoona
majina yao kwenda navitambulisho pamoja na kumbukumbu alizonazo
zitakazowezesha
dawati la malipo kufanyakazi kwa urahisi.
Aidha
Sadiki amemtaka mkurugenzi wa halimashauri ya manispaa yatemeke kutoa
matangazo
kwanjia ya vipaza sauti katika maeneu husika ilikuwafahamisha wanachi
juu
yazoezi hilo.
Tukio hilo lilitokea
aprili
2009 katika kambi ya jeshi la ulinzi la wananchi(JWTZ)ambapo mabo hayo
yalilipuka mfululizo nakusababisha vifo vya watu zaidi ya 20 na kujeruhi
200
huku mamia ya watu wakikosa makazi hali iliyosababisha watoto wengi
kupotea.
Hata hivyo mbali watu
kupoteza maisha katika tukio hilo
pia mabomu hayo yalisababisha uharibifu wakazi yawatu katika eneo hilo.