Na Kenneth
Ngelesi, Mbeya
LICHA ya Rais Jakaya Kikwete kuwaagiza
wakuu wa idara kutoa
taarifa kwa waandishi wa habari juu ya miradi ya Serikari hali hiyo
imekuwa
kinyume kwa halmashauri ya Mbeya vijijini baada
ya Kaimu Mkurugenzi Juliana
Lundama
kumtaka mratibu wa TASAF, Hadson
Mwasanyamba atoe taarifa za uongo
kwa vyombo vya habari.
Hali
hiyo imetokea
jana katika ofisi za Halmashauri ya Mbeya Vijijni baada ya waandishi
kufika
katika ofisi za Mkurugenzi kwa lengo la kutaka kupata taarifa za
utekelezaji wa
miradi mabalimblia ya maendeleo inayosimamiwa na mfuko wa maendeleo wa
TASAF.
Baada ya kufika katika ofisi hizo,
Lundama alidai kuwa hana
taarifa zozote za utekelezaji wa miradi kwani
yeye ana muda mfupi tangu kukaima nafasi hiyo iliyoachwa
wazi kutokana na Mkurugenzi
aliyekuja badala ya Juliana malange kuhamishiwa Halmashauri ya Moshi kurudi halmashauri kwake kwa ajili ya
kukabidhi.
Kaimu huiyo aliwataka waandishi wa
habari hao waenda kwa
wakuu wa idara ili kupatiwa taarifa sahihi jambo ambalo lilikuwa ni
danganya
toto.
Baadhi ya waandishi walifika
katika
ofisi za TASAF na kukutana na mkuu huyo wa idara ambaye alisema ili aweze
kutoa taarifa za utekezaji wa miradi hiyo anaitaji kujiridhisha kwa
kupata ruhusa kutoka kwa mkuu wake wa kazi.
Katika hali ya kushangazwa, Mkuu huyo
akiwa anawasiliana na
mratibu wa Tasaf kwa njia ya simu ya kiganjani, sauti ya simu hiyo ikiwa
juu
(Loud speker) sauti ya Kiongozi huyo ilisikika ikimtaka kiongozi huyo
kuwadanganya waajndishi hao.
“ Waandishi hao
wamekuja ofisini kwangu kutaka
taarifa mbalimbali zinazo husu miradi
ya maendeleo lakini nimewaeleza kwamba wawaone wakuu wa idara husika
kwani ndio
wanahizo taarifa kwani mimi sina taarifa sahihi kwa hiyo angalia namna
ya kuwa
danganya” ilisikika sauti ya Kaimu Mkurugenzi huyo.
Hatua hiyo imekuwa kinyume na maagizo
ya Rais Jakaya Kikwete
na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dr Nomad Sigalla aliye wataka watumishi wa
serikari
kutoa taarifa kwa wana habari hasa juu ya utekezaji wa miradi ya
maendeleo
inayo simamamiwa na serikari.
Mkuu wa mpya wa wilya ya Mbeya Dr
Nomadi Sigala wakati
akijitambulisha kwa wakuu wa idara hivi karibuni aliwataka wakuu wa
idara
kufanya kazi na waandishi wa habari kwani ndiyo njia pekee ya
kuwafamisha wanachi
kujua nini serikari yao inafanya.
Mwisho