UTOAJI WA
HUDUMA Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa wagonjwa unasusua
tokea kutangazwa kwa kuanza kwa mgomo huo Jumamosi ya wiki iliyopita Mgomo huo ulianza siku hiyo licha ya Mahakama ya Kazi kusitisha mgomo huo kuwa ni batili |
||
Huduma za kitabibu katika hospitali hiyo ni
finyu ukilinganisha na siku za nyuma kabla ya kutangazwa kwa mgomo huo Katika uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa kuna baadhi ya madaktari wanaendelea na kazi na hasa hususani wale bingwa Baadhi ya ndugu walionekana kushikwa na mgagasiko na kuhamisha wagonjwa wao kwa kujihami na kuokoa uhai wa ndugu zao waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo Katika wodi za hospitalini hapo wauguzi walionekana kuwepo licha ya kushindwa kufanya kazi kiufasaha kutokana na kutokuwepo kwa madaktari ambao wanategemeana katika kazi Katika wodi ya watoto ilisemekana na mmoja wa wauguzi kuwa, watoto wengi wanakufa kwa ukosefu wa hewa ya oksijeni wanapofanyiwa upasuaji kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kuvutia hewa. Baadhi ya wagonjwa kutoka mikoani wamekuwa wakiwa katika mazingira magumu kutokana na kutopata huduma stahiki Kwa mujibu wa Dkt. Ulimboka alisema huduma za dharura zitasitishwa katika hospitali hizo kutokana na serikali kutoonyesha nia ya kutatua madai yao kama ilivyotoa ahadi na badala yake kinachofanyika ni propaganda tu. Alisema kutokana na serikali kupuuza madai yao italazimika kuwajibika kikatiba katika suala la kuwahudumia wagonjwa ambao wataendelea kupata tabu kwa kukosa huduma za matibabu. Hata hivyo huduma katika hospitali na Amana, Temeke na Mwananyamala zinaonekana nazo kusuasua licha ya madaktari kuonekana maeneno yao ya kazi Licha ya kuripotiwa katika baadhi ya hospitali madaktari kuendelea na kazi nchini hali inayoonyehsa madaktari ksualitiana katika mgomo huo |
||
Na Pilly Kigome, Dar wa nifahamishe |
HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 19,2025
4 hours ago