Na Kenneth Ngelesi, Mbeya
MIILI ya watu kumi kati ya
kumi na watatu, waliofariki katika ajali mbaya iliyotokea kwenye kona iliyopo
mlima Mzalendo, kijiji cha Ntangano-Ijombe, imetambuliwa.
Ajali hiyo iliyotolkea juzi majira
ya saa 7:50 mchana, ilihusisha gari T.886 BDZ aina ya Toyota Coaster
lililokuwa limebeba abiria likielekea wilayani Kyela na gari T.658 ASJ aina ya
FAW likiwa na tela T.150 ASN, lililokuwa linatokea mpaka wa Kasumulu, wilayani
Kyela.
Muuguzi mkuu wa hospitali ya Rufaha Mbeya, Thomas Isdory, alisema hadi sasa
majeruhi saba wa ajali hiyo bado wanaendelea kupatiwa matibabu na hali zao
zinazidi kuimarika tofauti na walivyokuwa wamefikishwa siku ya tukio.
Isdory aliwataja marehemu
waliotambuliwa kuwa ni Lucia Livingstone (51), mkazi wa Katumba, Elenesta
Kikanga (62), ambaye ni mwalimu mstaafu na mkazi wa Ifunda mkoani Iringa.
Wengine ni Emmanuel Mwanjanja, mkazi
wa Ilomba, Pius Beye, mkazi wa Uyole, Mwase Pius, mkazi wa Ilomba jijini Mbeya
na dereva aliyekuwa anaendesha basi aina ya Coaster, Mwasa Daimond, mkazi wa
Iganzo jiji Mbeya.
Katika hatua nhingine muuguzi huyo
aliwataja marehemu wengine kuwa Lenah Ngomano (49), mkazi wa Rungwe, Bahati
Jafari (33), mkazi wa wilaya ya Kyela, Mwaniwe Fukasi (35), mkazi wa Uyole
mjini Mbeya na Yerusalem Mwakyusa (35), mkazi wa Mbeya mjini.
Muuguzi huoy mkuu aliwataja majeruhi wanaoendelea kupatiwa
matibabu hospitalini hapo kuwa Ford Mwakabungu (35), mkazi wa Kyela, Zainabu
Bahati (33), mkazi wa Igawilo na Catherine Komba (23), mkazi wa Hawelo.
Majeruhi wengine ni Neema
Mwakalukwa, mkazi wa Mlowo wilayani Mbozi, Paulina Francis (42), mkazi wa
Uyole, Esther Mgaya (21), mkazi wa Ujuni na Veronica Charles (57) mkazi wa
mkoani Iringa.
“Kwa kweli hali za majerui zinaendelea
vizuri ukilinganisha na huziu wakati wana letwa wengi wao hali zao zilikuwa mbaya
na bado wanaendelea kupatiwa matibabu” alisema Isdory.
eddymoblaze.blogspot.com ilifika katika
hospitalini hiyo na kushushuhudia
umati mkubwa wa wananchi waliokuwa wamefika kuchukua miili ya ndugu zao na
wengine kuja kuwatambua marehemu, hali iliyopelekea eneo hilo kugubikwa na
majonzi.