Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. John Mnyika (wa pili kushoto) akisubiri kusomewa hukumu katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam leo huku akiwa amekaa sambamba na mpinzani wake kwa tiketi ya CCM Bi. Hawa Ng’umbi (wa tatu kushoto).
Mashabiki wa Chama cha CHADEMA wakiwa wamefurika ndani ya Mahakama kuu jijini Dar es Salaam kusikiliza hukumu ya kesi ya Mh. John Mnyika.
Wengine walikosa nafasi na kuamua kusimama nje ya Lango kuu la Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Wafuasi wa Chama cha CHADEMA wakimpongeza Mh. John Mnyika mara baada ya kuibuka mshindi dhidi ya kesi iliyokuwa ikimkabili.
Mh. John Mnyika akiwa amebebwa juu juu na wafuasi wa Chama hicho pamoja na mashabiki wake nje ya Mahakama Kuu jijini Dar mara baada ya kushinda kesi yake iliyokuwa ikimkabili kuhusiana na Ushindi wake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
“Pole sana Mama ndio Siasa hiyo” Mmoja wa Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi akimpa pole Bi. Hawa Ng’umbi (katikati) mara baada ya kutoka Mahakamani.
Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi wakiwa na sura za huzuni baada ya kutoka Mahakamani.
Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe akifunguka na kuelezea furaha yake wakati wa mahojiano na Mwandishi wa ITV Godfrey Monyo nje ya Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam leo.
Maandamano ya wafuasi wa CHADEMA wakishangilia ushindi wa Mbunge John Mnyika wakielekea katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho.

Mh. John Mnyika ameshinda kesi ya kupinga ushindi wake katika Jimbo la Ubungo katika hukumu iliyotolewa leo na mahakama kuu ya Tanzania na kukifanya chama cha CHADEMA kuendelea kushikilia jimbo hilo.
Picha & Story kwa hisani ya MO Blog