Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Ndulamo wilayani Makete wamesema
ongezeko la pikipiki zinazofanya biashara ya kubeba abiria maarufu kama
bodaboda ni miongoni mwa kichocheo kinachosababisha unyanyasaji wa
kijinsia kwa wanafunzi hasa wa sekondari
Wakizungumza na mtandao huu kwa masharti ya kutotajwa majina yao wakazi hao wamesema madereva wengi wa bodaboda wamekuwa wakiwarubuni wanafunzi hasa wa kike kwa kuwapa 'lifti' wanapotoka au kwenda shuleni kwani kwa kiasi kikubwa wanafunzi hao hutembea umbali mrefu wakati wakitoka na kwenda shuleni
Wameongeza kuwa wakati mwingine mwanafunzi anachoka kutokana na kutembea umbali mrefu kila siku hivyo wakati wakiambiwa wapewe msaada na madereva bodaboda madereva hao pia hutumia mwanya huo huo kuwatongoza hivyo wanafunzi hao hukubali kwa kuwa hawana namna ya kukataa
Pia wamesema ukosefu wa mabweni kwa wanafunzi katika shule nyingi za sekondari hulazimisha wanafunzi hao kupanga mitaani hali inayopelekea kukutana na vishawishi mbalimbali hsa wanapokosa chakula na fedha kwa ajili ya pango la nyumba, hurubuniwa na kujikuta wakifanya ngono isiyosallama na wengi wao hupata mimba, na magonjwa ya ngono ikiwemo UKIMWI
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na mwandishi wetu alipokuwa akiandaa kipindi cha TUJADILIANE kinachorushwa na Kitulo FM kwa Ushirikiano wa shirika lisilo la kiserikali la SUMASESU ambalo pamoja na mambo mengine linalohusika na kutoa elimu ya ujinsia kwa wanafunzi kupitia proramu ya shule Salama