IDADI YA WANAWAKE WA WAFUGAJI WANAOGOMBEA NAFASI MBALIMBALI IMEONGEZEKA

NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE - MONDULI

Imeelezwa kuwa kwa sasa idadi ya wanawake kutoka jamii ya wafugaji ambao
wanajitokeza kuwania nafasi za uongozi mbalimbali katika jamii
imefikia asilimia 50 tofauti na hapo awali ambapo wanawake walikuwa na
mwitikio mdogo.

Hayo yameelezwa na Katibu wa umoja wa wanawake kupitia chama cha

mapinduzi(UWT) katika kata ya Engutoto, Bi Bihulda Kisaka wakati
aliopokuwa akiongea na Waandishi wa habari wilayani Monduli

Bi Kisaka alisema kuwa kilichofanya wanawake wengi wajitokeze hasa

katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho ni pamoja na uhamasishaji
ambao unafanywa na UWT wilaya ya monduli

Alifafanua kuwa kuongezeka kwa idadi ya wanawake hasa katika kata ya

Engutoto ni Motisha kubwa sana hasa kwa kata nyingine na jambo hilo
linatakiwa kuigwa na watu wengine

“Tuna idadi kubwa sana ya wanawake wa jamii ya wafugaji ambao

wanajitokeza katika kuomba nafasi mbalimbali tofauti na hapo awali
ambapo wengi walikuwa wanaogopa sana lakini sasa wengi wanajitokeza
sana”alisema Bi Kisaka

Pia aliongeza kuwa pamoja na kuwa wanawake wengi walikuwa wanajitokeza

hasa katika kata hiyo ya Engutoto bado  wanawake wanakabiliwa na
changamoto lukuki hali ambayo inachangia hata baadhi yao kushindwa
kutumia demokrasia yao vema

Mbali na hayo alitaja changamoto nyingine ni pamoja na uhaba wa fedha

hali ambayo nayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana washindwe kufikia
malengo yao mbalimbali hasa kwenye ulipaji wa ada

Awali aliwataka wanawake kuhakikisha kuwa wanatumia nafasi zao vema

kwa kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi
kwa kuwa wanahaki zao za msingi.
Na FULLSHANGWE


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo