Chama
cha Sauti ya Umma (SAU) kimempongeza Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh. John
Mnyika (Pichani) kwa ushindi aliyoupata katika kesi ya ubunge na
kumtaka achukulie kama changamoto za kisiasa na wala asijenge chuki
dhidi ya yeyote.
Katika
taarifa ya Chama hicho iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa
na Mwenyekiti wake Dakta Paul Kyara, imesema SAU wameguswa sana na suala
lililotokea katika jimbo hilo kwa sababu ofisi yao ya chama Makao Makuu
iko jimbo la Ubungo kwa hiyo Mh. Mnyika ni Mbunge wao na wana imani
naye.
Dakta
Paul Kyara amesema kwa niaba yake binafsi, viongozi wenzake, wanachama
pamoja na wafuasi wa SAU wanachukua nafasi hiyo kumpongeza Mwenyekiti wa
CHADEMA Taifa, viongozi wenzake, wanachama wa CHADEMA pamoja na wafuasi
wote wa CHADEMA nchi nzima na hasa wakazi wa Jimbo la Ubungo ambao ndio
walezi wa Mh.John Mnyika .
Na.MO BLOG TEAM