Na Kenneth Ngelesi, MBEYA
Wizara ya Mambo ya Ndani Kitengo cha Wakimbizi na Shirika la kuhudumia wakimbizi duniani (UNHCR) Ofisi Ndogo ya Mpanda wametakiwa kuelewa sheria za kimataifa, kikanda na kitaifa zinazolinda haki ya Mkimbizi.

Wito huo umetolewa leo jijini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abass Kandoro wakati akifungua semina elekezi kwa wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama iliyo fanyika katika Hitel ya Paradise jijini humo.
Amesema kuwa endapo viongozi hao wataelewa na kutambua sheria za kitaifa zinazolinda haki ya mkimbizi zitawezesha namna ya kutofautisha mkimbizi na mgeni toka nje ya nchi.
Amesema kumekuwepo na tabia ya kuwakamata wahamiaji haramu wengi ambao lengo lao si kuishi nchini bali ni kuvuka mipaka kwenda nchini nyingine kutafuta hali nzuri ya kiuchumi .
Mkuu huyo wa mkoa ameeleza kuwa pamoja na kuelewa vyema sheria hiyo ya ukimbizi nivema sasa wakatumia fursa hiyo katika kuongeza ubunifu na kujituma zaidi pamoja na kuandaa mapendekezo yatakayosaidia kupunguza tatizo la wakimbizi nchini.
Pia Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wajumbe hao pia kutoa mapendekezo yatakayo boresha utendaji wao wa kazi katika kuhudumia wakimbizi nchini.