Harakati za kuupinga muungano wa Tanganyika na Zanzibar zimeanza kuwatia tumbo joto wahusika visiwani Zanzibar katika wakati ambapo Tanzania iko katika mchakato wa kutafuta katiba mpya.
Wananchi wa Zanzibar sasa wapo katika harakati za kutafuta katiba mpya
Viongozi 12 wa harakati za kuupinga muungano huo wamekamatwa asubuhi ya leo na jeshi la polisi katika viwanja vya baraza la wawakilishi walikokuwa wamekwenda kwa lengo la kuwashindikiza wawakilishi waitishe kura hiyo ya maoni.
na DW