LUSHOTO
Serikali imetishia kuwafukuza kazi baadhi ya viongozi kuanzia ngazi ya vitongoji hadi kata wilayani Lushoto Mkoani Tanga kutokana na baadhi yao kushirikiana na baadhi ya wafanyabiashara kwa kuvuna na kusafirisha mbao ndani na nje ya nchi kinyume cha taratibu
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Lushoto Sophia Mjema katika kikao baina yake na viongozi wa serikali za vitongoji na vijiji kilichohudhuriwa pia na wadau wa misitu
Mkuu huyo wa wilaya amefafanua kuhusu tabia ya kufichiana siri kwa kuwalinda wahujumu misitu wa hifadhi ya asili ya wilaya ya Lushoto na hivyo amesema atakayekiuka agizo hilo sheria itachukua mkondo wake