MAKETE
Vijana wa wilaya ya Makete wameshauriwa kuacha tabia ya uvivu na kuchagua kazi, na badala yake kujiajiri wenyewe na kuacha tabia ya kuilaimu serikali kuwa ndiyo imesababisha ugumu wa maisha yao
Hayo yamezungumzwa na Afisa maendeleo ya jamii Bw. Denis Sinene wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii katika ofisi ya kijiji cha Iwawa wilayani Makete
Amewataka vijana hao kuachana na tabia hiyo na badala yake wanaweza kuanzisha vikundi vitakavyowasaidia kuinua vipato vyao na kuboresha maisha yao kwani kwa kufanya hivyo itakuwa rahisi kwao kupewa mikopo
Katika hatua nyingine amewaomba wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kutokomeza uhalifu unaofanywa na mtu binafsi au makundi hasi katika jamii
Na Obeth Ngajilo