Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Zainab Kwikwega
MAKETE
Wananchi wilayani Makete bila kujali itikadi zao wametakiwa kujitokeza kwa wingi kumpokea makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal ambaye anatarajiwa kufanya ziara ya kiserikali wilayani humo
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Zainab Ahmad Kwikwega wakati akizungumza na mwandishi wetu kuhusiana na ziara hiyo ya mh. makamu wa rais inayotarajiwa kufanyika wilayani hapo Jumatatu Februari 27 mwaka huu
Katika ziara hiyo Mh Makamu wa rais atapokelewa eneo la Mfumbi ambapo pamoja na mambo mengine ataweka jiwe la msingi kwenye soko la wakulima Mfumbi lililojengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na kuwasalimia wananchi watakaofika eneo hilo
Mbali na hilo pia Dk. Bilal ataweka jiwe la msingi kwenye nyumba ya walimu Kitulo Sekondari pamoja na kuhutubia wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi katika chuo cha VETA Makete pamoja na kuhutubia wananchi kwenye viwanja vya mabehewani Makete mjini
Mh. Kwikwega amewataka wananchi wa Makete kujitokeza kwa wingi kwani ziara hiyo ni ya maendeleo ya wananchi wote wa Makete na Taifa kwa ujumla
