MAKETE 23/02/2012
Jeshi la polisi wilayani Makete limetolea ufafanuzi tuhuma za kumuachia mtuhumiwa wa kesi ya kuwaweka kinyumba wanafunzi wawili wa shule ya sekondari Mwakavuta
Akizungumza na Kitulo fm Afisa upelelezi wa wilaya ASP Gozbert Komba amesema tuhuma hizo siyo sahihi kwa sababu mtuhumiwa aliachiwa kwa dhamana na upelelezi unaendelea
Malalamiko hayo yaliyolewa na mwananchi ambaye hakupenda kujitambulisha jina lake katika kipindi cha morning power kinachorushwa na kitulo Fm akidai sababu za wanafunzi kujihusisha na masuala ya uhusiano ya kimapenzi linatokana na mamlaka za kisheria kutokuwachukulia hatua watuhumiwa wa matukio hayo
Wakati huohuo polisi wametolea ufafanuzi kuwa suala la mvutano kati ya wananchi wa kijiji cha Isapulano na na mkazi wa kijiji hicho Bw.Silivyo Mahenge nakusema kuwa wamekwisha lishughulikia suala hilo na kwa sasa lipo mahakamani