MAKETE 23.02.2012
Imeelezwa kuwa mvua kubwa zinazoambatana na radi zinazoendelea kunyesha hivi sasa wilayani Makete ni miongoni mwa sababu zilizopelekea kukosekana kwa umeme siku mbili mfululizo Februari 19 na 20 wilayani hapa
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Meneja wa TANESCO wilayani Makete Bw. Zebedayo Gadau amesema mbali na mvua hizo pia baadhi ya wachungaji wa mifugo wamekuwa wakichezea nyaya za umeme kwa kutupa matawi ya miti hali inayopelekea hitilafu ya umeme na umeme kukatika
Pia Gadau alikanusha taarifa zilizozagaa miongoni mwa wananchi kuwa hitilafu hiyo ya umeme ilisababishwa na uwekaji wa transfoma katika chuo cha VETA Makete