HALELUYAAAAAAAAAAAAAAAAAAA!


Wakuu,Naandika nikiwa na majonzi sana juu tabia mpya ambapo siku hizi katika baadhi ya mabasa utakuta wanaingia wahubiri na kuanza kupiga kelele na kuhubiri juu ya Yesu na haja ya watu kuokoka.
 
Kwenye basi kuna kuwa na watu wengi wakiwemo waislamu,wahindu,wabudha,waconfisian,washinto,waenye dini za asili,wanaokana uwepo wa Mungu,wakristo wa madhehebu ya katoliki.
 
Lutherans,Anglicana ,wasabato ambao huwaona wahubiri hao kama manabii wa uongo na watu wapotoshaji,lakini kunakuwa na kundi la watu wanaowasikiliza yaani wenye kukubaliana na mahubiri yao.
 
Kunakuwa hata na watu wasiotambua uwepo wa mungu sembuse na wahubiri uchwara?.sasa inakuwa kero kwa myahudi au muislamu kuendelea(kulazimishwa) kusikiliza kwa zaidi ya saa moja maneno kwamba yesu ni mungu, upuuzi wa kusema watu waokoke na upuuzi kama huu.
 
Ni Kelele kwenda mbele, hakuna kuruhusu akili kutumika, wala hakuna maswali.Ingawa ninaouhakika kwamba hawa wahubiri uchwara hupanda magari haya bure, wanapotaka kushuka huomba michango eti nauli ya kurudi ubungo.
 
Hupretend kuomba nauli wakijua kuwa michango ya watu haiwezi kuishia nauli pekee.
 
Michango huzidi nauli na wakati watapanda bure kurudi ubungo labda wakipiga kelele humo pia wanazoziita mahubiri
 
Mimi ni mkristo lakini nakereka sana na wahubiri uchwara hawa kwani licha ya kupotosha mafundisho ya ukristo karibu yote wanatia kashfa dini hii kama warusi walivyopata kusema inaonekana kama bangi.
 
Kwa nini wamiliki wa magari wasiandike kwenye tiketi kwamba kwenye gari fulani kunakuwa na mahubiri ya wakristo wapentekoste(waliookoka???) ili wengine tusiotaka mambo hayo tusipande gari hizo kuliko mtu kuja akitaka kusafiri kisha akalazimika kuwa kanisani.
 
Je siku nyingine mtu akiamka na kuanza kukanusha upotoshaji huu, au akawa na mafundisho ambayo wengi hawayapendi mfano akasema dini yake inataka watoto wajamiiane na mama zao kama tendo la ubatizo na mengine kama hayo watu watamsikiliza tu bila kumshusha? na au mtu akiamua kupinga kitendo hicho kawa ni usumbufu hatakuwa na haki hiyo? hili limekaaje kimaadili? ni halali kulazimisha watu kusikiliza kitu wasichopenda kwenye usafiri wa umma? mimi napinga ujinga huu.
 
Na Mjegwablog


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo