MTAYARISHAJI na mwigizaji nyota wa Swahiliwood, Vincent Kigosi Ray the Greatest ameingiza vifaa vipya na vya kisasa kutoka nje baada ya kufanya safari katika nchi za Thailand na China.
Msanii huyo mwenye wapenzi wengi katika tasnia hiyo amesema teknolojia inakwenda kwa kasi na kwamba hayo yanaonekana mtu anapotoka nje.
Nimekuwa kila mwaka nikijiwekea malengo pamoja na kampuni yangu ya kuhakikisha kuwa tunakuwa mbele kwa kila hatua kwa suala nzima la utayarishaji bora, ndiyo maana mwaka huu nilisafiri kwenda China na Thailand kwa ajili ya ununuzi wa vifaa.
Ray ni msanii mbunifu na mpiganaji mwenye kuleta chachu za maendeleo kwa wasanii kwa kuwa mwasisi wa vitu vingi katika tasnia hiyo.
Kwa sasa kampuni yake ya RJ anayomiliki kwa kushirikiana na Blandina Chagula itakuwa na uwezo wa kutengeneza filamu zao na kazi za wasanii wengine kutokana na kuwa na vifaa vya kutosha.
Na Mwanaspoti