CHRISTINA MILLAN AJIUNGA CASH MONEY

Kundi la Cash Money,linazidi kujiozolea wasanii nchini marekani,mara baada  Christina Milian & Busta Rymes kutangazwa kujiunga na Young Cash Money,kuna habari kuwa,Rapper  Lil Wyne akiwa katika mahojiano na kituo kimoja cha radio Nchini  Marekani, amekubali kwamba mda wowote kuanzia sasa mwanamama Ashanti atajiunga na kundi lao.
Ashanti ambaye ni mwanachama wa kuni la Murder Inc anatarajiwa kusaini mkataba wa kujiunga na kundi hilo Lil Wyne akisikika akisema  “sitaki kuvuka mipaka yangu lakini nadhani tunafanya kazi na Ashanti sasa hivi”Mwaka jana Ashanti alifungua lebo yake inaitwa “Written Entertainment” ambayo kwa sasa ina dil na kuipromote single yake ya “The Woman You Love” aliyomshirikisha Busta Rymes wa Cash Money.
Ashanti alianza kushine wakati huo wa single kama za Wat’s love na Always on time akiwa na Ja Rule ambapo sasa hawapo tena kwenye lebo moja na wala hawashirikiani kama zamani, nakumbuka siku kadhaa zilizopita kabla Ja Rule hajaenda Jela, alitweet kwamba “nimejaribu kumwambia Ashanti tuungane kama zamani amekataa, ila simlaumu kwa sababu ni dada yangu na ninamuheshimu”


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo