MAKETE
Kikundi cha Walemavu Wilayani Makete (KICHAWAMA) kimewataka walemavu kote nchini kujishughulisha na shughuli mbalimbali zitakazowaingizia kipato ili waweze kujikimu kimaisha
Hayo yametamkwa na Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw. Niko Mbwillo wakatia akizungumza na Kitulo Fm na kusema kuwa ipo dhana potofu iliyojengeka kwa jamii na walemavu wenyewe kuwa wao hawawezi chochote jambo ambalo amelikanusha na kuwataka wajishughulishe
Bw. Mbwilo amesema ni vizuri kujishughulisha katika shughuli mbalimbali bila kujali ulemavu walio nao ili kuidhihirishia jamii kuwa walemavu wanaweza
Amezitaja changamoto alizonazo katika biashara yake kwa sasa kuwa ni pamoja na ukosefu wa usafirishaji wa bidhaa zake kwani kwa kiasi kikubwa wateja wake wapo Iringa mjini pamoja na miti aina ya mianzi ambayo anaitumia kama malighafi kupatwa na ugonjwa ambao husababisha miti hiyo kukauka
Hata hivyo ameishukuru idara ya Udiakonia chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa kuwawezesha na kuwapa mshikamano mzuri walemavu wilayani Makete pamoja na elimu ya Ujasiriamali waliyonayo walemavu
Kikundi hicho cha KICHAWAMA kina jumla ya walemavu 30 ambapo wengi wao hujihusisha na shughuli mbalimbali zinazowaingizia kipato.