Chama cha upinzani Chadema mkoani Mbeya imeanza mikutano ya hadhara leo katika Kata ya Nzovwe, huku aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo hilo kwa vipindi viwili mfululizo, Joseph Mbilinyi 'Sugu' akitangaza kumtaka Mbunge wa sasa Dk Tulia Akson, katika kinyang’anyiro hicho.
Katika mfululizo wa mikutano hiyo ambayo imeanzia kata ya Uyole, Sugu ndiye anaonekana kuwa kinara huku akipewa hamasa na viongozi wengine wa chama hicho mkoani humo.
"Tunakutaka Tulia, tunakutaka Tulia, tunakutaka Tulia" ni kauli Sugu akielezea mjadala ulioibuka juu ya kugawanya kwa jimbo Mbeya mjini, mapendekezo yanayosemekana kuwasiliwa na Dk Tulia ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sugu ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 10, (2010-20) kabla ya uchaguzi Mkuu uliopita kuchukuliwa na Dk Tulia Ackson ambaye pia ni spika wa bunge kwa sasa.
Akizungumza jana Alhamisi Mei 11 kwenye mkutano huo Sugu amesema alisikia hoja hiyo lakini hakuwahi kulielezea popote akisisitiza kuwa yeye analitaka Jimbo la Mbeya mjini.
Amesema yeye akiwa Mbunge aliweza kuzihudumia Kata zote 36 za Jimbo hilo, lakini anashangaa hoja ya kuligawa na kwamba vyovyote iwavyo anamtaka Dk Tulia Ackson popote.
"Nashangaa kwanini huyu spika anapaniki tu, mimi sijaongea chochote tayari ameanza kuzungumzia hili jambo, sasa nasema hivi tukutane 2025 kwani aliyemuweka bungeni kwa sasa hayupo tena"