Shabiki wa Yanga aitwaye Jane, mkazi wa Kata ya Bwilingu Huko Chalinze mkoa wa Pwani, amepoteza maisha wakati akiangalia mchezo wa jana wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga.
Imeelezwa kuwa shabiki huyo alipatwa na presha na kuanguka ghafla.
Katika mchezo huo uliopigwa Aprili 16, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ulishuhudia Simba wakimaliza uteja wa miaka mitatu kwa kuitandika Yanga mabao 2-0, ambayo yalipachikwa na Inonga Baka na Kibu Denis.