Mapya mradi wa Maji Tandala wa Milioni 200

Kero ya upatikanaji wa maji ya bomba katika kijiji cha Tandala wilayani Makete mkoani Njombe inaendelea kutatuliwa na serikali ambapo utekelezaji wa mradi wa maji wa Tsh. milioni 200 utaanza utekelezwaji wake muda wowote kuanzia sasa


Katika mkutano wa hadhara wa kijiji hicho uliofanyika Aprili 6,2023 Meneja wa RUWASA wilaya ya Makete Mhandisi Innocent Lyamuya amesema fedha hizo ni kwa ajili ya upanuzi wa mradi wa maji Tandala na utekelezaji wake ni kwa mfumo wa "Force Account" yaani ukihusisha serikali kushirikiana na mafundi wa eneo husika na sio ule wa kutumia mkandarasi

Mhandisi Lyamuya amesema kwa sasa yapo ambayo tayari yameshafanyika ikiwemo ununuzi wa vifaa vya ujenzi ambavyo vitaanza kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo wa maji, hivyo kwa kuwaomba wananchi kutoa nguvu kazi pale itakapohitajika ikiwemo kusaidia kusogeza vifaa vya ujenzi eneo husika

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Tandala Yusuph Ilomo amewahimiza wananchi hao kutoa ushirikiano ili mradi huo ukamilike kama serikali ilivyopanga ambapo pia amemuomba fundi mkuu kuwatumia mafundi wa kijiji hicho huku baadhi ya wananchi wakishukuru kwa mradi huo ambao wanategemea utakuwa mkombozi kwao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo