Muliro: Msiogope kuomba lifti kwenye difenda za polisi


 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amewataka wananchi kuacha woga wa kuomba lifti kwenye difenda za polisi kwa kile alichokieleza kuwa gari hizo ni mali ya umma.


Ameyasema hayo leo Februari 14, 2023 wakati wa mahojiano katika kipindi cha Clouds360 kinachorushwa na televisheni ya Clouds.

“Kuna mtu alishawahi kuomba lift kwenye Difenda hakupewa? Kwanini wanapanda watuhumiwa tu. Kwanini raia wa kawaida hawaombi lift? Au walishawahi kulisimamisha wakanyimwa lift? kwa mfano Difenda linakwenda Bunju, Tegeta, Kunduchu, Kitunda au Mwanagati, Kivule analiona kabisa limeandikwa Polisi na wewe unakwenda maeneo hayo kwanini usilisimamishe ukaomba lift?,

Hayo magari ya umma kwani polisi ni nini? Si ni Taasisi ya Umma? Jaribu siku kulisimamisha kama utanyimwa lift",” alisema Muliro.

Kauli yake iliibua hisia tofauti kutoka kwa wafuatiliaji wa kipindi hicho ambapo kupitia mitandao ya kijamii walitoa mitazamo yao huku wengine wakienda mbali zaidi na kumtaka atoe namba za simu ili ikitokea vinginevyo wampigie simu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo