Wanafunzi kadhaa walilazwa hospitalini Jumatatu, Januari 9, 2023 alasiri baada ya kula chakula chao cha mchana uliotolewa na serikali.
Wanafunzi hao wa Shule ya Msingi ya Mandalpur, wanaripotiwa kuathirika baada ya kula chakula hicho kilichokuwa na nyoka.
Maafisa walisema kuwa takriban wanafunzi 20 kati ya 53 waliokuwepo shuleni wakati huo, walikula chakula hicho. Lakini kulikuwa na hofu baada ya mfanyakazi wa shule hiyo aliyepika chakula cha mchana kudai kuwa nyoka allipatikana kwenye chombo kimoja kilichokuwa pojo.
"Watoto wote walikimbizwa mara moja katika Hospitali ya Rampurhat baada ya kuugua.Wanawake wawili waliokuwa wanapika walimwona nyoka walipokuwa wakipakuwa dengu. Mmoja wao au wawili walikuwa wameiweka tu kinywani mwao." "Baada ya kumuona nyoka huyo, kila mtu aliombwa aache kula," mwalimu mkuu Nimai Chandra Dey alisema. Habari hizo zilipoenea mtaani, wanakijiji wenye hasira walikusanyika shuleni humo na kuharibu gari la mwalimu mkuu.
Wanafunzi hao waliruhisiwa kwenda nyumbani baada ya kutibiwa na wako katika hali sawa kiafya.
Chanzo:TUKO