Wamcharukia Mchungaji aliyewatimua wasimamizi wa Ndoa

Baadhi ya jamaa wa bibi harusi kutoka Nyamira wamejitokeza kukemea pasta aliyefukuza wasimamizi kutokana na mavazi yao.


Hii ni baada ya kisa kimoja kutoka Nyamira ambapo mhubiri aliamua kuwafurusha wasimamizi ambao si wa kanisa la SDA.


Mhubiri huyo alisema wasimamizi hao walikuwa wamevalia kwa namna ambayo si ya kupendeza Mwenye Mungu. Damaris Obiero amesema kisa hicho kilitopkea katika harusi ya dadake Roselyn Barongo na akakosoa mhubiri wa siku.


Alisema pasta huyo aliharibu siku ambayo ilifaa kuwa kubwa katika maisha ya dadake na hivyo kuonya Wakenya dhidi ya kumhusisha katika harusi nyingine. "Huyu mhubiri aliharibu harusi ya dadangu. Alisema kila mtu ambaye si wa SDA hafai kushiriki harusi hiyo. Wasimamizi hawakushiriki. Maneno ilikuwa inatoka mdomo wake ndio ilifanya watu wakasirike," alisema kipusa huyo


Aliwataka Wakenya kumtafuta mhubiri huyo iwapo wanataka siku yao ya harusi kuharibika kama vile ilifanyika ya dadake. "Anaitwa Jared Omwoyo kutoka Eldoret, sasa wewe mtafute katika harusi yako iwapo unataka mambo kuenda fyongo," aliongeza dada huyo. Katika video iliyosambaa mtandaoni, pasta huyo aliskika akisema hatakubali kuendesha harusi ambapo kina dada wana mavazi fulani.


Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo