Mikutano ya Hadhara ya Vyama vya Siasa Yaruhusiwa


Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameondoa rasmi tangazo la kuzuia mikutano ya hadhara na kuruhusu vyama vya siasa kuanza kufanya mikutano hiyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni


Rais Samia ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es salaam wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa nchini ambapo amesema ni haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na kuwataka kutumia nafasi hivyo kufanya siasa za kistaraabu na za kujenga badala ya kubomoa nchi


"Wajibu wenu vyama vya siasa ni kufuata sheria na kanuni zinavyosema, lakini kama waungwana na wastarabu niwaombe sana tunatoa ruhusa ya mikutano, twendeni tukafanye siasa za kistarabu, za kupevuka na kujenga na si kubomoa"


Aidha Rais Samia amesisitiza kuwa utaratibu wa kufanya mikutano hiyo utaendelea kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi ili kupata vibali huku akisema kwa hali ilivyo sasa vibali hivyo vitaruhusiwa


"Ni haki kwa vyama vya siasa kuendesha mikutano yao ya hadhara, lakini ndugu zangu tuna wajibu, kwa serikali wajibu wetu ni kulinda mikutano ya vyama vya siasa, mnatupa taarifa kama sheria inavyosema, vyombo vinatoa ruhusa, wakiona kuna hatari hawatoi ruhusa, lakini kwa hatua tuliyofika ruhusa za kufanya mikutano zitatolewa"


Katika hatua nyingine Rais Samia amesema hivi karibuni ataunda kamati maalumu kwa ajili ya kushauri kuhusu marekebisho ya katiba mpya na njia bora ya kuliendea jambo hilo huku akisisitiza kuwa mchakato huo utakuwa wa kistaraabu ili kupata katiba bora ya watanzania.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo