Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amewataka raia wa nchini humo kuacha kuchunguza simu za wapenzi wao.
Wito wake ukionekana kuwa sehemu ya ombi la kujaribu kupunguza viwango vya talaka nchini.
Takwimu zinaonyesha kuwa nchi hiyo ilirekodi zaidi ya kesi 22,000 za talaka mwaka jana pekee, takwimu ambazo rais alizitaja kuwa za kusikitisha.
Ukosefu wa haki za ndoa, uzinzi, unyanyasaji wa kijinsia, matusi na ukatili ni miongoni mwa sababu zilizotolewa mahakamani katika kesi zinazohusu talaka.