Mwalimu anaswa akiiba nguo za ndani za walimu wenzake

Mwalimu mmoja wa kike ambaye alikuwa miongoni mwa walimu wa kusahihisha mitihani ya kitaifa ya KCSE katika shule ya kitaifa ya Alliance alinaswa kwenye video akiiba chupi za walimu wenzao.

Katika video iliyosambaa siku ya Alhamisi, mtahini huyo wa kike ambaye ni mwalimu wa Kiswahili anaonekana akiokota nguo kwenye Kamba ya kuning'inia iliojumuisha nguo za ndani, taulo za usoni na blauzi.

Mwalimu huyo aliiba nguo zenye maji zilizokuwa zimetundikwa kwenye kamba. Baadaye iliripotiwa kuwa mtahini huyo ni mwalimu wa Kiswahili kutoka mojawapo ya shule bora nchini.

Maafisa wa usalama katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Alliance pia walithibitisha kuwa mtahini huyo aliombwa kuandika rasmi taarifa kuhusu madai ambayo yaliletwa dhidi yake.

Waathiriwa pia waliitwa kutambua nguo ambazo zilichukuliwa kutoka kwa Kamba ya nguo nyuma ya bweni la wasichana. Maafisa wa usalama wa shule hiyo pia waliripoti kisa hicho kwa Kituo cha Polisi cha Kiambu ambao walifanya uchunguzi.

Hata hivyo, haijabainika iwapo mwalimu huyo wa kike atashtakiwa mahakamani au ataonywa na kusamehewa.

Tukio hili linajiri wiki chache baada ya afisa wa polisi aliyekuwa akilinda mitihani ya kitaifa ikifanyika mwezi Desemba pia akioonekana kwenye kanda za CCTV akichokora mikoba ya walimu na kuiba vilivyokuwemo ndani wakati shughuli ya mitihani ilikuwa inaendelea katika shule moja.

JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo