Makubwa tena kwenye sakata la Dogo wa miaka 17 kuwapa mimba wanawake 10

Mvulana wa miaka 17 amekamatwa na polisi akituhumiwa kuwapachika mimba wanawake kumi nchini Nigeria.


Noble Uzuchi amekamatwa pamoja na mshukiwa mwenzake Chigozie Ogbonna mwenye umri wa miaka 29 baada ya polisi wa River State kugundua kampuni ya 'kutengeneza watoto' eneo hilo.


Kwa mujibu wa polisi, Uzuchi, Ogbonna na wanawakw wengine wawili Favour Bright, 30 na Peace Alikoi, 40 walikuwa wakiendesha kampuni hiyo ya 'kutengeneza watoto'. Shirika la habari la Nigeria kwa jina PUNCH limeripoti kuwa msemaji wa polisi Grace Iringe-Koko alisema kuwa wanaume hao wawili walilipewa jukumu la kuwatimia mimba wanawake hao kwa kushiriki nao ngono kwa muda mrefu.


Uchunguzi wa mwanzo ulifichua kuwa Alikoi alikuwa kiongozi wa kundi hilo. Baada ya kuwatunga mimba wanawake hao, Alikoi angebaki na watoto kisha kuwalipa wanawake hao takriban shilingi 140,000. Iringe-Koko anasema kuwa polisi walipata ujumbe kutoka kwa raia kuhusu kampuni hiyo na wakazama kazini mara moja. Oparesheni ya kuwasaka na kuwanasa wanunuzi wa watoto hao inaendelea ili wajibu mashtaka ya uhalifu huo.


Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo