Amfumania Mkewe Mjamzito akichepuka Katika Kitanda cha Hospitali

Mwanaume raia wa Uganda alipigwa na butwaa baada ya kumpata mkewe mjamzito ambaye alikuwa amelazwa hospitalini akifanya mapenzi na barobaro wa miaka 24.


Mwanamke huyo alifumaniwa na mumewe alipokwenda kumjulia hali katika Hospitali ya Apac ambako alikuwa amekaa kwa siku tano kwa sababu ya kuugua malaria.


Alex Okuta, mkazi wa Kijiji cha Abwal “A” katika kaunti ndogo ya Chegere kutoka Wilaya ya Apac alithibitisha kwamba mkewe mgonjwa alimchiti. "Nilifanya ziara ya kushtukiza hospitalini kummwangalia mke wangu ndipo nikampata jamaa huyo kitandani na mke wangu mjamzito," alifichua, na kuongeza kuwa mke wake "amelazwa kwa sababu alikuwa anaugua malaria."


Daily Monitor inaripoti kwamba awali, polisi katika Wilaya ya Apac hawakuwa na shtaka la la kumfungulia kijana huyo anayeishi kuchoma nyama katika Jiji la Apac. "Tumependekeza mashtaka ya kusababisha kero ya umma dhidi ya mshukiwa, lakini bado tunachunguza na tutawajulisha kwa wakati unaofaa," ilisema ripoti ya Alhamisi, Januari 13.


Mshtakiwa alipenya katika wadi ya wanawake wiki jana na Joseph Onuk, msimamizi wa Hospitali ya Apac, alijutia kisa hicho ambacho anaamini kingeweza kuepukwa mara ya kwanza. "Ninamlaumu mume wa mwanamke huyo," alisema. “Unawezaje kumpeleka mkeo hospitali na kuchukua muda mrefu bila kuja kumuona? Wanaume wengine kila wakati wanasema kuwa wana shughuli nyingi. Mtu ambaye hana shughuli nyingi atamnyang'anya mkeo," alisema. Mwaka jana, bado jamaa mwingine alijikuta katika hali ya kizungumkuti mkee alipomfichulia ana mimba ya mwanamume mwingine.


Jamaa huyo aliomba ushauri kutoka kwa watu mitandoani kwani mpenzi alimsihi asimteme akiahidi kumpeleka mtoto huyo kwa babake pindi tu atakapozaliwa.


Kila mmoja wao alikuwa na hisia mseto baadhi wakionesha kuchanganyikiwa huku wengine nao wakionesha imani mambo yatakuiwa sawa.


Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo