Jeshi la polisi mkoa wa Pwani linamshikilia mtu mmoja aliefahamika kwa jina moja la Michael akituhumiwa kuhusika na kifo cha utata cha anayedaiwa kuwa ni mke wake marehemu Primsrose Matsambire mwenye umri wa miaka (39) raia wa Zimbabwe
Primrose amefariki dunia katika hospitali ya Rufaa ya Tumbi iliyopo Mkoa wa Pwani Januari 11/2023 alipopelekwa kupatiwa matibabu baada ya kukutwa akiwa anatokwa damu mdomoni akiwa nyumbani kwake Kiluvya Madukani Wilayani Kisarawe
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Pwani Pius Lutumo ameeleza kuwa aliyebaini tukio la marehemu kutokwa damu kwa wingi mdomoni ni msichana wa kazi ambaye baada ya kuona hali aliyonayo mwajiri wake huyo (marehemu) aliondoka moja kwa moja mpaka kwa majirani ili kuomba msaada na walipofika walimpeleka katika hospitali ya Tumbi kwaajili ya matibabu.
ACP Lutumo amesema mume wa marehemu hakuwepo wakati tukio hilo likitokea
Jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye ni mume wa marehemu kwaajili ya mahojiano
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Tumbi huku jeshi la polis likiendelea na uchunguzi wa kifo cha utata cha mwanamke huyo raia wa Zimbabwe