Waziri Ummy awatembelea majeruhi wa ajali ya Basi la Arusha Express

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo amewatembelea majeruhi wa ajali ya Basi la Arusha Express lililogongana na Lori, Mzakwe Dodoma. Majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na wanaendelea vyema na matibabu.
Waziri Ummy amesema Hospitali hiyo ilipokea Majeruhi 21 ambapo hadi kufikia leo Majeruhi mmoja ambaye alipatwa na majeraha makubwa amefariki kufanya idadi ya waliofariki kufikia watu 7, watu 9 wameruhusiwa kuondoka na 11 wanaendelea na vyema na matibabu.

Amewashukuru watumishi wa Hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa na majeruhi wa ajali hiyo iliyotokea.





JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo