Bodaboda afariki dunia kwa kupigwa

MWANAUME anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 36, ambaye hakufahamika kwa haraka amekutwa amefariki dunia katika eneo la Maji machafu, Kijiji cha Nyabange wilayani Butiama.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Longinus Tibishubwamu, ametaja kuwa chanzo cha kifo hicho kuwa ni tamaa ya mali, kwakuwa Pikipiki aliyokuwa akiiendesha iliibwa katika tukio hilo la Novemba 16 Mwaka huu.

Amesema, marehemu alipigwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali kichwani, shingoni na tumboni na kumsababishia majeraha ambayo ndiyo yanayosadikiwa kumsababishia kifo.

Kamanda huyo amesema Jeshi la Polisi bado linaendelea na upelelezi wa tukio hilo, lakini taarifa za awali zinaeleza mtu huyo alikuwa akifanya shughuli za bodaboda mjini Musoma.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo