Waliomfanyia unyama wa kutisha mtoto wapandishwa kizimbani

Watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakikabiliwa na tuhuma kadhaa ikiwemo kumshambulia mtoto wa miaka 15 kwa kumchapa viboko vilivyomsabishia maumivu na majeraha mwilini mwake


Taarifa za awali zinabainisha kuwa Binti huyo alipigwa na mwanaume anaetajwa kuwa ni mume wake, Namendea Lesiria akishirikiana na  rafiki yake kwa kile kilichodaiwa ni kumwaga dawa ya nyama ya mbuzi tukio ambalo limetoka Septemba 2022.


Waliofikishwa mahakamani ni mume wa binti huyo Namendea Lesiria Pamoja na  rafiki yake  wote wakiwa ni wakazi wa kijiji cha Gelailumbwa Wilayani Longido Mkoani Arusha.


Kesi hiyo inasikilizwa kwa Faragha ikiwa hatua za ushahidi, na itaendelea Oktoba 20 Mwaka huu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo