Mwanafunzi achomwa mikono, ashindwa kufanya Mtihani wa Darasa la 7


Mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Shahende mkoani Geita Helema Helena Mashaka (13), ameshindwa kutimiza ndoto yake baada ya mama yake kumchoma moto mikono kwa tuhuma za kuiba sh.30,000.


Edgar Michael ni mtendaji wa kijiji Bukoli amesema kuwa tukio hilo limetokea katika kata ya Butobela, mkoani Geita, majira ya saa 2 asubuhi, baada ya mama yake kumtuhumu kuiba kiasi hicho cha fedha.


Amesema alipata taarifa ya mtoto huyo kujeruhiwa kutoka kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo akidai kuwa kuna binti amechomwa moto na mama yake na ameshindwa kufanya mitihani.


Mwenyekiti huyo alianza kumfuatilia mzazi wa binti huyo na kisha kumkamata na kudai alifanya kitendo hicho kwa sababu mtoto huyo aliiba sh. 30,000.


“Mpaka sasa mzazi huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo kidogo cha Polisi kilichopo Kata ya Bukoli, na mwanafunzi amepelekwa Zahanati ya Bukoli kwa ajili ya kupatiwa matibabu.


Aidha Mtendaji huyo amesema taratibu zinaendelea ili mwanafunzi huyo aweze kupata nafasi ya kurudia kufanya mitihani hiyo ya kuhitimu kwa mwaka 2023.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo