Mama aliyewatoroka watoto wake wadogo, arudi nyumbani

Mama wa watoto wanne waliotelekezwa katika mtaa wa mabanda wa Mukuru Kwa Njenga nchini Kenya alirejea Alhamisi, Oktoba 27 usiku, saa chache baada ya ombi lao la kutaka usaidizi kupamba vichwa vya habari kitaifa.


Kulingana na mama wa watoto hao Lucy Adaki, nyakati ngumu za kiuchumi zilimlazimu kuwaacha wanawe na kwenda kutafuta kazi ya kuwakimu mahitaji yao. 


Maafisa kutoka idara ya huduma za kijamii, familia na watoto walisema wana hao waliachwa na mama yao huku kaunti ikiendelea na shughuli ya kuwawezesha kurejea shuleni.

"Sikuwa na namna. Hakuna jinsi ningewatazama wakifa kwa njaa na nimekaa tu. Njia pekee niliyokuwa nayo ni kwenda nje na kuwaletea chochote nitakachopata," alisema.

Adaki pia alichukua fursa hiyo kuomba ajira kutoka kwa gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja. "Huyu mama anawajibika sana na ana akili timamu, ila tu amekosa ajira ndiposa apate pesa za kulipa kodi," alisema mmoja wa viongozi hao, Robert Mwema.

Maafisa hao waliapa kuhakikisha watoto hao wanapta lishe na mahitaji yao mengine yanashughulikiwa. "Nimekuwa nikiwaona watoto hawa karibu na mlango, na ninapoangalia hali zao, ni kama wana njaa. Labda niwanunulie ndizi ili wale," jirani alisema. "Nilidhani wakati wanazurura tu mlangoni, labda mama yao ameenda kazini au amechelewa kurudi na labda atachelewa kupika," jirani huyo anayejali aliongeza. Hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa mama huyo ambaye ni mgeni katika eneo hilo kuwaacha wanawe pekee yao.

Majirani wengine wamejitokeza kuwasaidia watoto hao kwa chakula na mahitaji mengine baada ya mama yao kukosa kazi. Wengine walilaumu gharama ya juu ya maisha kuwa sababu mojawapo ya mama huyo kukimbia na kuacha burungutu la furaha nyuma.

Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo