Atangaza kumlipa fedha Mwanaume atakayeweza kumpa Mimba

Mwanamke ambaye anatamani kuwa na mtoto ameanza msako wa kumtafuta barobaro mtanashati ambaye atampachika ujauzito.


Mshawishi wa mitandao ya kijamii Uwaoma Susan Joseph alishiriki ombi la mwanamke huyo kwenye Facebook, na utambulisho wake haukujulikana.


Huku mwanamke huyo tajiri akitoa kitita cha KSh 831,000 kwa mwanamume atakeangukia bahati, kulikuwa na masharti fulani. Susan aliandika kwamba mwanamke huyo alisema barobaro huyo atafumbwa macho wakati wa kujamiiana. Pia atalipiwa makazi kwa muda na kuachiliwa tu baada ya ujauzito kuthibitishwa.


Kiini cha kufumba macho ni kumzuia asije kumtafuta yeye na mtoto hapo baadaye. Chapisho la Susan linasema: "Suzy naomba unichapishie "Nahitaji mwanaume ambaye atanipa ujauzito, awe mtanashati.. "Atafumbwa macho, ataingia na kufanya mapenzi na mimi, baada ya hapo nitamlipa, kufumba macho ni kwamba asije kunitafuta na mtoto baadaye ,nitampangishia makazi mpaka nithibitishe kuwa nina mimba ndipo aweze kuondoka. Kwa sasa ninaishi Abuja na gharama zote zitakuwa juu yangu.


Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo